Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibu mambo ni moto

Kibu Denis Wa Moto.jpeg Kibu Denis akifunga bao juzi kwenye mchezo wa kirafiki

Sun, 30 Jul 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kibu Denis juzi alifunga bao la pili kwenye mechi za kujipima ngumu kwa Simba iliyopo kambini Uturuki na kumfanya kocha wa timu hiyo Roberto Oliveira 'Robertinho' kushindwa kujizuia na kusema jamaa anazidi kuimarika na amemsisitizia kukomaa zaidi kabla yua msimu mpya haujaanza.

Simba imecheza michezo mitatu zikiwa ni za kujiandaa na msimu mpya ikiwa huko Uturuki, ikianza na sare kabla ya juzi kuvaana na Turan PFK mara mbili ikainza mapema kuifunga mabao 2-0 kisha jioni kufungwa 1-0, lakini akaunti ya Kibu ikiwa na mabao mawili na huilo limempagawisha kocha.

Akizungumza Robertinho alisema anafurahia viwango vya wachezaji katika maandalizi, huku akisema i faraja kwake kuona wachezaji wake wakionyesha mabadiliko huku ari ya ushindani ikiwa juu kwa mchezaji mmoja mmoja.

"Nimekuwa nikiongea na mchezaji mmoja mmoja kwa lengo la kuimarisha kiwango chake, naamini (Kibu) anaweza kufanya zaidi, unajibikaji wake ni mkubwa pamoja na wachezaji wenzake, tunaendelea vizuri na maandalizi na ni wazi kila mmoja anajua tunapaswa kucheza kwa namna gani," alisema kocha huyo wa kimataifa wa Brazil na kuongeza;

"Huwa nafurahia kuona kila mchezaji akiwa na uwezo mzuri wa kufunga kwa sababu kuna mechi ambazo mshambuliaji wetu wa mwisho anaweza kudhibitiwa, tunatakiwa kutotabirika kama timu yeyote ambaye anapata nafasi anatakiwa kuitumia, tupo katika hatua nzuri kama timu."

Akiongelea kiwango cha timu yake kwenye mchezo wa pili wa kirafiki waliopoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Turan PFK alisema vijana wake walifanya kazi nzuri kwenye kushambulia, kuzuia na kumiliki kwa muda mrefu.

“Kwangu siangalii matokeo ya mwisho bali mchezo wenyewe ulivyokuwa.Tumecheza vizuri kuanzia mwanzo hadi mwisho. Wachezaji wameonekana wapo timamu kimwili, kimbinu na hilo ni jambo ambalo limenifurahisha,” alisema kocha huyo.

Robertinho ameweka wazi kuwa anahitaji kucheza mechi nyingine moja ya kirafiki mwishoni mwa juma kabla ya timu kurejea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya tamasha la Simba Day, Agosti 6,2023.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: