Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibu atimiza ndoto yake Kimataifa

Kibu Dennisa CAF Kibu Denis

Tue, 15 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Wekundu wa Msimbazi Kibu Denis, ameweka wazi furaha yake ya kucheza mchezo wake wa kwanza wa Kimataifa kwa ngazi ya Klabu katika mchezo dhidi ya RS Berkane , Mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Kibu ambaye usajili wake wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ulichelewa hivyo alishindwa kucheza mechi za awali na mchezo wa jumapili ulikuwa mchezo wake wa kwanza pia baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yanamkabili.

Kibu anasema kila mchezaji furaha yake ni kucheza mechi kubwa za Afrika kama ilivyokuwa Jumapili na anaamini ataendelea kuaminiwa na kocha katika michezo inayofuata.

"Ni furaha kubwa kwangu kucheza mechi yangu ya kwanza ya Kimataifa ya Mashindano kwa ngazi ya Klabu. Kila mchezaji anatamani kupata nafasi ya kucheza michuano hii, naamini mwalimu ataendelea kunipa nafasi" amesema Kibu

Kibu alipata majeraha katika mchezo dhidi ya Mbeya City uliopigwa Uwanja wa Sokoine, Januari 16 ambapo alikosekana Uwanjani kwa takribani wiki saba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live