Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibu Mkandaji na hadithi ya kinyago kumtisha aliyekichonga

KIBU DENISS Kibu Mkandaji na hadithi ya kinyago kumtisha aliyekichonga

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkandaji Kibu Dennis ambaye kwa sasa anapambania hali yake kurejea kwenye ubora ameibua jambo ndani ya Simba baada ya tetesi kueleza kwamba ana ofa kutoka timu inayoshiriki Ligi Kuu Bara.

Kibu mchezo uliopita dhidi ya Namungo alikwama kukamilisha dakika 90 kuna hatihati akakosekana kwenye mchezo wa kesho Mei 3 2024 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Taarifa zinaeleza kuwa mabosi wa Simba walizungumza naye kumpa mkataba mpya na wakafikia naye kwenye maslahi mazuri lakini akagoma kusaini.

Mkataba wake unagota mwisho mwishoni mwa msimu hivyo kama hatasaini dili jipya ataondoka bure.

Msimu wa 2023/24 ndani ya ligi amefunga bao moja na kutoa pasi tatu za mabao ni chaguo la kwanza ndani ya Simba eneo la kiungo mshambuliaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live