Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibu Denis, roho ya Simba katikati ya hukumu ya leo na kesho

Kibu Denis Prosper Kibu Denis

Mon, 6 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dunia ya mpira inatuchanganya. Na inazidi kutuchanganya. Ni vita ya muda mrefu kati takwimu na juhudi/kiwango cha mchezaji. Ni vita ambayo kila shabiki wa mpira ameibeba kwa maono na hoja zake za msingi.

Kila mtu anaweza kuwa sahihi kwa mtazamo wake. Ule mjadala wa nani bora kati ya Zinedine Zidane na Kelvin Debruyne ndio uliibuka hapa. Wanaosema De bruyne ni bora zaidi watakuja wamebeba takwimu za assits ambazo zitakuacha mdomo wazi.

Yule anayesema Zidane ni bora zaidi yeye atakuja na zile video za kombe la dunia zikimuonyesha Zidane akiwanyanyasa Wabrazil kiwango chake kitakufanya upigwe na butwaa.

Ni miaka mitatu imepita Luis Diaz ndani ya Epl ana assist 10 na magoli 16 tu. Ni magoli ambayo Vinius jr anafunga kwenye mechi 15 tu ndani ya msimu mmoja. Lakini Luis Diaz bado anaimbwa ndani ya Liverpool.

Bernado Silva haujezi kumuona kwenye takwimu za magoli wala assists. Lakini ndio miongoni mwa wachezaji bora kwa Pep Gurdiola.

Wapo watakao mhukumu Kibu Denis kwa takwimu zake, wapo watakaomlaki kwa kiwango chake bora. Wote watakuja na hoja zao na utazikubali. Mpira unachanganya, hauwezi kuacha kutuchanganya.

Ila ukweli ni kwamba kwenye orodha ya wachezaji watatu bora kwa simba msimu huu jina la kibu Denis linaweza kushika nafasi ya pili, tone la jasho lake linaacha alama ya upambanaji kila leo.

Hukumu ya Kibu Denis ipo kwenye mahakama ya Pilato, Simba Sc ni muda kuchagua kusuka au kunyoa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live