Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibu Denis kamili kuivaa Mtibwa Sugar

Kibu D Na Robertinho Kibu Denis kamili kuivaa Mtibwa Sugar

Fri, 10 Mar 2023 Chanzo: Dar24

Kiungo Mshambuliaji wa Simba SC Kibu Denis huenda akawa sehemu ya kikosi cha timu hiyo katika mchezo wa kesho dhidi ya Mtibwa Sugar, utakaopigwa Uwanja wa Manungu Complex.

Tayari Simba SC imeshawasili mjini Morogoro kwa mchezo huo wa Mzunguuko wa 24 wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambao utapigwa kesho kuanzia saa kumi jioni.

Kibu aliumia kwenye mchezo wa Kundi C kati ya Simba SC na Vipers uliyopigwa mwishoni mwa mwezi Februari mjini Entebbe – Uganda na kushinda 1-0 na kumfanya akose mchezo wa Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ dhidi ya Africans Sports na mchezo wa Jumanne (Machi 07) wa marudiano dhidi ya Vipers, lakini kwa sasa yu tayari kuivaa Mtibwa Sugar.

Kocha mkuu wa Simba SC, Oliveira Roberto Robertinho amesema; “Kibu ni moja ya wachezaji wapambanaji kikosini, aliumia kidogo lakini kwa sasa yupo tayari na amekuwa akifanya mazoezi na timu.”

“Mchezo ujayo tunacheza na Mtibwa Sugar, kuna baadhi ya wachezaji tutawapumzisha na wengine wasiopata nafasi mara kwa mara wataonekana.”

Tangu ujio wa Kocha huyo kutoka Brazil, Kibu amekuwa miongoni mwa mastaa wanaopata muda mwingi wa kucheza kikosini hapo na Simba kesho itaingia uwanjani ikiwa kumbukumbu nzuri ya kutopoteza michezo saba ya mwisho iliyokutana na Mtibwa Sugar, ikishinda tano na kutoa sare mbili.

Chanzo: Dar24