Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibu Denis hana maajabu zaidi ya kuifunga Yanga

Kibu Kuwasili.jpeg Kibu Denis.

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kibu Denis anakataa Tsh milioni 588 za Simba SC kwa sababu aliifunga Yanga Africa kwenye Mechi ambayo Simba Sports kafungwa 5-1, Novemba 5, 2023.

Na aliwafunga tena Yanga Africa kwenye Ile Mechi Simba Sports alishinda 2-0 Aprili 16, 2023.

Ni Sababu hiyo tu ,hakuna nyingine. Kibu Denis Kwa roho yake ya upambanaji ni mchezaji wa Kukujengea Msingi wa team tu (Floor Raiser) Sio mchezaji wa Kumtegemea Kushinda Vikombe (Ceiling Raiser).

Yani ni Kama unajenga nyumba tu huyu ni mchezaji anakutengenezea Foundation. Lakini huwezi Kuishi kwenye nyumba ambayo ipo kwenye Foundation.

Floor Raiser Players ni aina ya wachezaji wenye uwezo wa kuitoa team kwenye hali mbaya na Kupata ahueni. Kibu Denis anaipa Simba Sports ahueni, wajisikie vizuri kwenye baadhi ya mechi.

Nyumba siku zote ni kwenye Finishing (Ceiling Raiser Players). Hawa ndo wachezaji wenye uwezo wa Kuitoa team kwenye ahueni Mpka kwenye team ya ushindani wa Vikombe.

Ceiling Raiser Players mara nyingi ndo wachezaji Ghali zaidi Duniani.Hawa ndo wachezaji ambao huwa wanadengua sana kwenye Usajili .Sio Kibu Denis.

Na don't get me Wrong,sisemi ni mchezaji Mbaya Kabisa.Lakini sio mchezaji unaweza Kumtegemea kama unataka Kutengeneza team ya Kushinda Makombe na kufika nusu fainali ya CAF Champions League.

Unaikumbuka Yanga Africa ya Kumtegemea Deus Kaseke na Ditram Nchimbi (Duma) hao ni Floor Raiser Players). Yanga Africa imetoka huko imeleta Ceiling Raiser Players (Paccome Zouzoua, Stephanie Aziz, Maxi Nzengeli).

So kwanini anawadengulia Simba Sports? Simba wanaweza Kuingia kwenye Mkenge Kwamba anatakiwa na team nyingine ya Dar es salaam ili apige Pesa nyingi tu.

Lakini kwa Maoni Yangu sio mchezaji wa Kuidengulia Simba Sports na Kukataa Mil 558.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live