Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibu Denis, Dilunga Hali Mbaya Simba

REVIEW Kibu Denis (600 X 400) Kibu Denis, Dilunga Hali Mbaya Simba

Thu, 10 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MENEJA Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amefungukia maendeleo ya wachezaji wao Kibu Denis na Hassan Dilunga ambao kwa sasa ni majeruhi.

Hiyo ni katika kuelekea mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi dhidi ya Asec Mimosas utakaochezwa Jumapili ya wiki hii kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Ally amesema: “Leo (jana) asubuhi Dilunga ameenda kuangaliwa tatizo lake na kujua ni kwa muda gani atakaa nje ya uwanja.

“Kwa upande wa Kibu, yeye bado hali yake siyo nzuri, ila Taddeo Lwanga amesharejea na kuanza mazoezi na timu na huenda mwalimu akamtumia katika mchezo wa Jumapili.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live