Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibu D arejea dimbani, kuwavaa Horoya Jumamosi!

KIBU D AREJEA Kibu D arejea dimbani, kuwavaa Horoya Jumamosi!

Mon, 13 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Good news kwa Wekundu wa Msimbazi Simba SC ni kwamba, Kiungo wao Mshambuliaji Kibu Denis 'Kibu D' amerejea kikosini akiwa amepona na yupo fiti kwa asilimia mia.

Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally amesema, Kibu amerejea kikosini na tayari ameajiunga na wenzake kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa tano wa hatua ya makundi utakaopigwa Jumamosi hii (Marchi 18) kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar dhidi ya Horoya ya Guinea.

"Habari njema, njema zaidi ni kwamba Kibu D amerejea kikosi na yupo fiti asilimia mia. Ni mechi ngumu tunakwenda kucheza Jumamosi hii lakini ni mechi ambayo tumewekeza nguvu na akili zetu zote tuweze kushinda ili tuweze kufuzu robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika," alisema Ahmed.

Ahmed alimalizia kwa kusema, wachezaji wengine waliokuwa majeruhi kama Okrah na Sawadogo, wataendelea kuukosa mchezo huo lakini nyote wengine wote waliosalia, wapo fiti kwa ajili ya mchezo huo.

Kibu D aliumia kwenye mchezo dhidi ya Vipers SC nchini Uganda mchezo wao wa awali walioshinda goli 1-0 na mchezo wa marudiano wa hatua hiyo ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika uliopigwa Benjamini Mkapa jijini Dar, Simba aliendeleza ubabe kwa kumtandika kwa mara nyingine, goli 1-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live