Kibegi chenye jezi mpya ya Simba SC kimewasili Marangu mkoani Kilimanjaro tayari kwa ajili ya kukipandishwa kilele cha Mlima Kilimanjaro na kutambulisha jezi mpya zitakazotumika msimu wa 2023/2024.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ali aliondoka jana na kibegi hicho kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani humo.
Picha mbalimbali zilizochapishwa leo kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ya timu hiyo zimemuonesha Ahmed akiwa kwenye amewasili Kilimanjaro na kibegi hicho.
Zoezi la kukipandisha kibegi hicho litaanza leo, Ijumaa jezi mpya za timu hiyo zitatambulishwa.
Itakumbukwa, huu ni muendelezo wa klabu hiyo katika kutangaza utalii wa Tanzania ambapo kwa misimu kadhaa jezi zinazotumika na klabu hiyo hususani katika michuano ya kimataifa zimekuwa na mchoro wa Mlima Kilimanjaro pamoja na maandishi yakuchombeza kutembelea mlima huo ‘Visit Kilimanjaro’.