Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibarua cha Ole Gunnar Solskjaer ndani ya United kipo salama

Gettyimages 1346916187 Kocha wa Man United, Ole Gunner Solkjaer

Tue, 26 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ole Gunnar Solskjaer ataendelea kubakia kocha wa kikosi cha united katika mchezo wao ujao wa Ligi dhidi ya Tottenham siku ya jumammosi, Licha ya wachezaji ndani ya kikosi hicho kuonekana kupoteza imani nae.

Ripoti zinadai kuwa kutokana na kipigo cha aibu ilichokipata mwishoni mwa juma kutoka kwa Liverpool, walitegemea mabosi wangelichukulia suala hilo kwa uzito mkubwa na kuachana na kocha huyo.

Lakini baada ya vikao vya siku mbili na majadiliano, taarifa zinaeleza kuwa mabosi wa juu ndani ya klabu, wamempa nafasi M-norway huyo kubadili mambo ndani ya klabu licha ya yote yanayoendelea ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo.

Inadaiwa kuwa wachezaji wa United wamepoteza imani na uwezo wa Solskjaer kimbinu kushindana na makocha mahiri ndani ya EPL, wakichanganywa na maelekezo yake kimbinu.

Mashabiki na wapenzi wa Manchester United kwa sasa kutoka kila pembe ya Dunia, hakuna wanachokitaka kukisikia kwa sasa zaidi ya taarifa ya kuondolewa kwa Ole ndani ya United.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live