Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibadeni awapa somo wazawa Ligi Kuu

Kibaden Abdallah Kibaden

Thu, 28 Sep 2023 Chanzo: Dar24

Wachezaji Nassoro Kapama, Hussein Kazi na Crispin Ngushi ni kati ya wachezaji wa Simba SC na Young Africans wanaokabiliwa na mtihani wa kupambana kutoboa, kwani inaoenekana kwa sasa kazini kuna kazi kupata nafasi ya kucheza.

Kapama ni mchezaji kiraka aliyesajiliwa msimu uliopita kutoka Kagera Sugar na hadi sasa hana uhakika wa namba Msimbazi sawa na mshambuliaji Mohamed Mussa ambaye tangu alipofunga dhidi ya Coastal Union mechi ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) hajasikika tena.

Wachezaji hao sambamba na Hussein Kazi hajapewa nafasi, lakini upande wa kiungo yupo Mzamiru Yassan na Sadio Kanoute ambao viwango vyao vipo juu.

Mussa anakabiliwa na ushindani wa wazoefu kina Jean Baleke aliyefunga mara tano Ligi Kuu, Moses Phiri (bao moja), Willy Onana (moja), hivyo anatakiwa kukaza buti.

Japo pia kuna nahodha John Bocco, lakini rekodi zinambeba kwani tangu 2008/09 alipofunga bao moja hakuna msimu ambao hajafunga, hivyo ni suala la muda.

Kwa Young Africans, Ngushi na Denis Nkane majeraha yamekuwa yakiwasumbua, hivyo wana kazi ya kupambana kuonyesha uwezo, jambo ambalo limemfanya kocha wa zamani wa Simba SC, Abdallah Kibadeni kuwataka kujiamini na kukaza buti.

“Kwanza lazima wawe na mazoezi ya ziada ili makocha wakiona washawishike nao, wajiamini hadi wanasajiliwa walionyesha uwezo walikotoka, jambo la msingi zaidi wasijibweteke,” amesema

Chanzo: Dar24