Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibadeni atoa tamko Afcon

40374 Pic+kibaden Kibadeni atoa tamko Afcon

Wed, 6 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17, ‘Serengeti Boys’ ikipangwa kucheza na Guinea, Australia na Uturuki kwenye mashindano ya Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa), wadau wa soka wamesema mechi hizo ni kipimo kizuri kwa timu hiyo.

Serengeti Boys itacheza na Guinea Machi 4, itavaana na Australia Machi 6 kabla ya kucheza na Uturuki Machi 8 mjini Antalya, Uturuki.

Mashindano hayo ambayo yatashirikisha mataifa 17, yana lengo la kuzipa mazoezi na uzoefu timu zinazokabiliwa na mashindano tofauti ikiwemo Serengeti Boys ambayo itakuwa mwenyeji kwenye fainali za Afrika (Afcon) zitakazofanyika Aprili, Dar es Salaam.

Kocha wa zamani wa Simba, Abdallah Kibadeni alisema mashindano hayo yatawaongezea maarifa Serengeti Boys.

“Uturuki watakutana na timu zenye uzoefu zinazotoka nchi zilizoendelea, kama watatumia ipasavyo mashindano hayo yatawajenga kushindana katika Afcon,” alisema Kibadeni.

Kocha wa Mwadui, Ally Bizimungu alisema ni fursa nzuri ya maandalizi na wakitumia vyema mashindano hayo yatawajenga na kocha atatumia kutambua kasoro kabla ya kuanza fainali hizo.

Kipa wa zamani wa Simba Idd Pazi alisema ushiriki wao katika mashindano hayo utasaidia kuwasoma washindani wao katika Afcon.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ammy Ninje alisema wachezaji 30 wa Serengeti Boys wapo kambini Dar es Salaam kujiandaa na mashindano hayo. Fainali za Afcon zinatarajiwa kuanza Aprili 14 hadi 28.



Chanzo: mwananchi.co.tz