Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibabage aongeza kandarasi Yanga

Kibabage Ms Kibabage aongeza kandarasi Yanga

Thu, 4 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa kushoto Nickson Clement Kibabage ameongeza mkataba wa miaka mitatu kuendelea kuitumikia Klabu ya Young Africans SC.

Hiyo ni katika kuendelea kuboresha kikosi hicho kuelekea msimu ujao wa 2024-2025.

Kibabage ambaye amekuwa na uwezo wa kuzuia na kupandisha mashambulizi kutokea upande wa kushoto, alijiunga na Young Africans SC mwanzoni mwa msimu wa 2023-2024

Akiwa ndani ya Young Africans ambapo amecheza kwa msimu mmoja, amebeba ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC na Kombe la CRDB Bank Federation, huku pia akiwemo katika mafanikio ya timu iliyocheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2023-2024

Nickson Kibabage amekuwa na mchango mkubwa kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu NBC msimu uliopita wa 2023/24 na ukiwa msimu wake wa kwanza alimaliza akiwa na “assist” tano.

Katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha kubwa, uongozi wa Yanga unaendelea kuboresha kikosi kwa kusajili wachezaji wapya na kuwaongezea mikataba wale ambao benchi la ufundi likiongozwa na Mwalimu Miguel Gamondi limependekeza waendelee kuwepo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live