Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibabage: Robo fainali tunatoboa

Kibabage  2048x1462 Kibabage: Robo fainali tunatoboa

Wed, 20 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea mchezo wa leo Jumatano wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya timu ya Yanga SC dhidi ya Medeama, beki wa kushoto wa Yanga, Nickson Kibabage qmesema kuwa wachezaji wote wamejiandaa kikamilifu kwa ajili ya kupambana na kuhakikisha kupata ushindi kwenye mchezo huo ili kufufua matumaini ya kwenda robo fainali.

Kibabage amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya wachezaji wenzake kuelekea mchezo huo.

Leo Jumatano, Yanga itakuwa mwenyeji wa Medeama katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika Kundi D utakaochezwa kuanzia saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

“Kwa upande wetu sisi wachezaji tumejiandaa vizuri na kikubwa kila mchezaji anatambua umuhimu wa mchezo wa kesho (leo) kwa sababu mchezo wa kesho unahitaji pointi tatu ili tuwe nafasi nzuri katika kundi.

“Hapo awali malengo yalikuwa ni kuingia kwenye makundi na nafasi hiyo tumefanikiwa, ukiangalia hata katika kundi letu nafasi ya kufuzu ipo kwa sababu nina Imani katika mchezo huo wachezaji wote wanatambua na wanahitaji kufuzu hatua inayofuata. Nina Imani tutafanya vizuri katika mchezo wetu.

“Wachezaji tumejiandaa kwa ajili ya mchezo kwa sababu tunaamini tukipata alama tatu tutakuwa na alama tano, huku tukiwa na mchezo mwingine nyumbani dhidi ya CR Belouizdad, kwa hiyo tuna Imani tutafanya vizuri zaidi kuwapa furaha mashabiki wetu.

“Mwalimu ameona, kwenye makosa tushafanyia kazi mazoezini, nina imani katika mchezo wa kesho tutafanya vizuri zaidi.”

Yanga inahitaji ushindi katika mchezo huo ili kufufua matumaini ya kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya hivi sasa kuwa na alama mbili zilizotokana na kucheza mechi tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live