Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibabage, Pacome na Mudathir kuchuana Tuzo ya NIC

Pacome Mudathir Kibabage Kibabage, Pacome na Mudathir kuchuana Tuzo ya NIC

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji watatu wa Klabu ya Yanga waliochaguliwa kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Februari 2024 ni Mudathir Yahya, Pacome Zouzoua na Nickson Kibabage.

Kwa mwezi Februari, takwimu zinaonesha kuwa, Mudathir alifunga magoli matano, Pacome magoli mawili na asisti moja, huku Kibabage akiwa na asisti tatu pekee.

Ikumbukwe kwamba, tuzo hiyo inatolewa na Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwa kushirikiana na Klabu yetu ya Young Africans.

Mashabiki na wanachama wa Yanga ndiyo wenye jukumu la kupiga kura kupitia Application ya Yanga SC, ili kumpata mshindi wa tuzo hiyo.

Tuzo hizo zimeanza kutolewa mwezi Oktoba 2023 chini ya udhamini wa NIC, ambapo mpaka sasa washindi wanne wamepatikana.

Washindi hao ni Stephane Aziz Ki (Oktoba), Pacome Zouzoua (Novemba), Djigui Diarra (Desemba) na Clement Mzize (Januari).

Washindi wote wa tuzo hizo, kila mmoja amekabidhiwa kitita cha shilingi milioni nne kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: