Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibabage: Ndoto yangu imetimia

Kibabage Na Mtototot Kibabage: Ndoto yangu imetimia

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa kushoto wa Yanga SC, Nickson Kibabage amesema ametimiza ndoto yake ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC akiwa na msimu mmoja tu ndani ya Young Africans.

Kibabage ambaye alijiunga na kikosi ya Yanga mwanzoni mwa msimu huu akitokea Singida Fountain Gate, amesema ndani ya Young Africans kuna vingi amejifunza huku akimshukuru Kocha Miguel Gamondi kwa kumsaidia kuzidi kuwa bora.

“Kwanza namshukuru Mungu ulikuwa msimu mzuri kwangu na ni mara ya kwanza kucheza timu kubwa na ndoto yangu imetimia kuchukua ubingwa.

“Kocha Miguel Gamondi huwa ananiambia niwe mtulivu kwa sababu ninacheza na mtu mwenye uzoefu na nijifunze kutokana na yeye kwani kuna wakati huwa nafanya makosa ananikumbusha.

“Naweza kusema Gamondi ni kocha mzuri ambaye ananipa nafasi na ananiambia nionyeshe uwezo wangu.

“Kibwana, Job na Mshery naweza kusema ni mawakala wangu na wao ndiyo waliofanikisha mimi kuja hapa kwani waliniambia hapa ndiyo sehemu sahihi na leo nimetimiza ndoto yangu nikiwa na wanangu ambao nilipambana nao tangu tukiwa wadogo.

“Nawashukuru Wananchi kwa sapoti yao kwa sababu hawajanionyesha unyonge, ninapopata nafasi wanakuwa na mimi ninavyocheza vizuri na hata pale ninapocheza vibaya wananiambia niongeze juhudi zaidi, kwa hiyo ni watu ambao wamehusika kwa kiwango kikubwa kwangu msimu huu. Nawapenda sana,” alisema Kibabage.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live