Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibabage: Msiseme Wazawa Tumefeli Changamoto Ni Nyingi

Simon Msuva Na Nickson Kibabage Kibabage: Msiseme Wazawa Tumefeli Changamoto Ni Nyingi

Tue, 8 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Tanzania, Nickson Kibabage anayekipiga KMC, amesema miongoni mwa sababu kubwa iliyomfanya arejee nchini kutoka klabu ya Difaa el Jadidi ya Morocco timu aliyowahi kuichezea Simon Msuva ni Ubaguzi wa rangi.

“Kuna muda unavumilia hadi unaona inatosha, wenzetu ni wabinafsi sana ila wengi wa mashabiki zetu hawalijui hili hivyo kubaki na kauli ya mchezaji fulani kashindwa huko ughaibuni,” amesema Kibabage na kuongeza;

“Ilifika mahala unakuta wanaogelea sehemu kisha nawe unajiandaa kuungana nao ila ukiingia tu unaona wachezaji wote wanatoka wanakuacha mwenyewe, yaani unabaki na maswali mengi yasiyokuwa na majibu hivyo mwishoni nikaona inatosha.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live