Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiatu cha Aziz Ki; Yanga haina cha kupoteza

Kazi Aziz Ki 4 04 23 At 13.jpeg Kiatu cha Aziz Ki; Yanga haina cha kupoteza

Tue, 21 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hivi majuzi Msemaji wa Klabu Simba, Ahmed Ally aliwashangaza wadau wa soka nchini baada ya kuweka bayana kuwa timu hiyo inamuunga mkono mchezaji wa Azam Fc, Feisal Salum atwae tuzo ya mfungaji bora msimu huu.

Feisal amefunga mabao 15 akiwa sawa na Aziz Ki wa Yanga lakini Ki akiwa na assists nane akiongoza sawa na Kipre Junior wa Azam Fc.

Katika misimu miwili iliyopita Yanga ilipigwa vita kali kuhakikisha haitoi mfungaji bora hasa baada ya kuwa imetwaa ubingwa.

Hata msimu uliopita Saido Ntibazonkiza alipigiwa chapuo ya kushinda kiatu cha dhahabu akiwa amefunga mabao 17 sawa na Fiston Mayele licha ya kuwa Saido alifunga mabao mengi ya penati.

Baada ya Aziz Ki kufungana magoli na Feisal tayari tumeona kanuni imetangazwa kuwa msimu huu kama wafungaji bora watakuwa wawili au zaidi yule atakayekuwa amefunga mabao machache ya penati ndio ataondoka na tuzo.

Na ikatokea kigezo hicho kikashindwa kuamua basi yule aliyecheza dakika chache zaidi atabeba tuzo.

Katika mechi tatu zilizobaki Yanga haina cha kupoteza kwani tayari imetwaa ubingwa, kazi iliyobaki sasa ni kuhakikisha Aziz Ki anaibuka mfungaji bora.

Aziz Ki amekuwa na mchango mkubwa katika ubingwa wa Yanga msimu huu anastahili kushinda tuzo nje ya ubingwa huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: