Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Khomeny, Nashon wasepa Ihefu

Kevin Nashon Ee Kelvin Nashon

Sun, 14 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji wa Singida Fountain Gate, Abubakari Khomeny na Kelvin Nashon wamejiunga kwa mkopo wa miezi sita katika kikosi cha Ihefu.

Khomeny anayecheza nafasi ya kipa hajawa na wakati mzuri katika kikosi cha Singida tangu msimu uanze hali ambayo imemlazimu kutoka kwa mkopo ili kupata changamoto mpya.

Kipa huyo ameshindwa kufua dafu mbele ya makipa wenzake Ibrahim Rashid ‘Parapanda’, Benedict Haule ‘Beko’ na Beno Kakolanya.

Khomeny msimu huu hajadaka mchezo wowote ule wa mashindano akiwa na kikosi hicho cha Singida FG.

Kwenda kwake Ihefu kunaenda kuongeza nguvu eneo la kipa ambalo wapo Fikirini Bakari, Hussein Masalanga na Haroun Mandanda.

Ihefu hadi sasa imeruhusu mabao 17 huku ikifunga mabao 10.

Upande wa kiungo Nashon yeye mwanzoni mwa msimu alikuwa anacheza kwa mkopo katika kikosi cha Mtibwa Sugar na sasa anageukia Ihefu.

Lengo la kwenda Ihefu ni kuongeza nguvu kwenye kiungo ukabaji ambapo nafasi hiyo alikuwa anacheza Shaban Msala ambaye msimu uliopita alikuwa katika kikosi cha Ruvu Shooting iliyoshuka daraja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live