Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Khomeiny Aboubakar ni Mwananchi

Komeyy At 11 Khomeiny Aboubakar

Mon, 8 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imemtambulisha golikipa mpya, Khomeiny Aboubakar kutoka Singida Black Stars zamani Ihefu kwa mkataba miaka miwili.

Aboubakar (25) ameongezwa kwenye orodha ya walinda mlango wa kikosi cha Yanga baada ya Metacha Mnata kumaliza mkataba na kupewa mkono wa kwa heri.

Yanga itakuwa na magolkipa Djigui Diarra, Abutwalib Mshery na ingizo jipya Khomeiny Aboubakar.

Huu ni usajili wa nne kwenye timu hiyo katika dirisha hili la usajili baada ya awali kuwanasa Clatous Chama, Prince Dube na Chadrack Boka.



Yanga wamemtambulisha kipa huyo kupitia Yanga App;

"Kipa Khomeiny Aboubakar Khomeiny rasmi ni Mwananchi baada ya kujiunga na Young Africans SC akitokea Ihefu FC.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 25, anakuja kuungana na Djigui Diarra na Aboutwalib Mshery katika kulinda lango la mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC na Kombe la Shirikisho la CRDB Bank.

Ujio wa Khomeiny ni sehemu ya kuboresha kikosi chetu kuelekea msimu ujao ambapo tunaamini uwepo wake utaongeza kitu cha tofauti.



Hiyo inatokana na uzoefu wake na msingi bora wa kisoka alionao kutokana na kucheza timu zote za taifa za Tanzania za vijana ikiwemo U-20 na U-23.

Khomeiny anakuwa mchezaji wa nne mpya kutambulishwa ndani ya Young Africans SC baada ya kiungo Clatous Chama, mshambuliaji Prince Dube na beki wa kushoto Chadrack Boka,"
imesema taarifa ya Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live