Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Khan akanusha Bayern kumsajili Ronaldo

Oliver Khna Turn CEO wa Bayern akanusha usajili wa Ronaldo

Wed, 30 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Cristiano Ronaldo baada ya kutangazwa kuachwa na klabu ya Manchester United, habari nyingi ziliibuka kuwa Mshambuliaji huyo wa Ureno anahusishwa kuhitajika na miamba ya Ujerumani Bayern Munich.

Sasa ni kwamba, Aliyekuwa CEO wa Bayern Munich Oliver Kahn ameweka wazi uvumi wa habari hizo kuhusu klabu yake kumhitaji Ronaldo ambaye kwa sasa ni mchezaji huru, amesema kuwa Bayern haitamsajili Cristiano.

“Bayern Haitamsajili Cristiano Ronaldo, Naweza kuondoa uwezekano wa kumnunua Ronaldo. Tumezingatia, sote tunampenda Ronaldo lakini mkakati wetu ni tofauti. Tuna falsafa safi na mipango mizuri ya jinsi timu yetu inapaswa kuwa”.

Klabu ya Manchester United ilitangaza kuachana na mchezaji huoy, kwa makubaliano ya pande zote mbili, hii inatokana na mahojiano aliyoyafanya wiki moja kabla ya michuano ya kombe la dunia kuanza, ambapo alieleza kuwa United ilimsaliti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live