Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kevin De Bruyne awaburuza Salah, Son EPL

0 JS265944657 Kevin De Bruyne

Sat, 21 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Manchester City, Kevin de Bruyne ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Raia huyo wa Ubelgiji anajivunia kiwango bora msimu huu akifunga mabao 15 na pasi zilizozaa mabao 7.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29, alitwaa tuzo hiyo mwaka 2020.

Tuzo hiyo inachukuliwa na mchezaji wa Manchester City kwa msimu wa tatu mfululizo kufuatia Ruben Diaz kukabidhiwa msimu iliopita na kwa mara ya mwisho nyota tofauti na wa The Citizen kuitwaa ni Mohamed Salah wa Liverpool mwaka 2018.

Mohamed Salah na Heuing-Min Son ambao wapo katika kinyang'anyiro cha tuzo ya mfungaji bora,walikuwa ni miongoni mwa majina ya wachezaji 8 waliokuwa wakiwania tuzo hiyo.

Nyota wengine waliokuwa wakiwania tuzo hiyo ni Joao Cancelo(Man City)Trent Alexander Anold(Liverpool),Jarrod Bowen(West Ham United),Bukayo Saka(Arsenal) na James Ward-Prows (Southampton).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live