Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Ubakaji ya Dani Alves kusikilizwa leo

Dani Alves Pp Beki wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Brazil, Dani Alves

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa zamani wa Barcelona na PSG, Dani Alves anatarajiwa kufikishwa Mahakamani Jumatatu hii huko Barcelona kwa tuhuma za kumbaka msichana huko Sutton kwenye klabu ya usiku katika Mji Mkuu wa Catalonia mnamo Desemba 30, 2022.

Kesi hiyo imepangwa kusilizwa kwa siku tatu na karibu mashahidi thelathini wataitwa kutoa ushahidi wao.

Mchezaji huyo ambaye amekaa kizuizini kwa muda wa mwaka mmoja, hapo awali alikana kukutana na msichana huyo, lakini kutokana na kuzidiwa na ushahidi , sasa anadai uhusiano huo ulikuwa wa makubaliano na kwamba alikuwa amelewa.

Mwathiriwa huyo ambaye alikuwa na umri wa miaka 21 wakati tukio hilo linatokea, anadai kuwa alimpiga kofi na kumfungia kwenye vyoo vya eneo la VIP kwenye klabu hiyo ya usiku kabla ya tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live