Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi kibao zinamalizwa wikiendi hii

Wsw Kesi kibao zinamalizwa wikiendi hii

Sat, 11 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Real Madrid imeshabeba ubingwa wa La Liga msimu huu na kumaliza mjadala wa kuhusu mbio za ubingwa wa taji hilo. Wakati kesi ya ubingwa wa La Liga ikifungwa, vita nyingine imeibuka kwenye ligi hiyo.

Mchakamchaka wa La Liga unaingia kwenye mechi za raundi ya 35, huku wikiendi hii ikitarajia kutoa majibu ya maswali kibao ya kuhusu nani kavuna nini kwenye vita hiyo ya La Liga kwa msimu huu.

Kasheshe lilianzia jana Ijumaa kwa miamba inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo, Girona kwenda kukipiga na Alaves ugenini.

Girona ilikwenda kwenye mechi hiyo ikiwa na mzuka wa kuichapa Barcelona mabao 4-2 katika mchezo wao uliopita.

Ushindi huo uliihakikishia Girona tiketi ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, wakati walipowang’oa Barcelona kwenye nafasi ya pili na kuwashusha kwenye nafasi ya tatu. Jambo hilo liliwafanya Girona pia kukamatia tiketi ya kucheza Spanish Supercup huko Saudi Arabia msimu ujao.

Girona inahitaji ushindi katika mchezo huo ili kujihakikishia nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo hasa baada ya kuwa na uhakika wa kuhusu tiketi ya kucheza Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Villarreal kichapo chao kutoka kwa Celta Vigo wikiendi iliyopita kilionekana kufuta ndoto zao za kufuzu michuano ya Ulaya msimu ujao, watakuwa na kibarua cha kuikabili Sevilla, ambao hawana presha yoyote ya kushuka daraja, hivyo mechi hiyo itakuwa ya heshima tu.

Mechi ya Mallorca nyumbani dhidi ya Las Palmas itakuwa na mambo ya kutazamwa, ambapo wenyeji Mallorca waliopo kwenye nafasi ya nne kutoka mkiani, pointi sita juu ya Cadiz inayoshika nafasi ya mwisho kwa zile timu zinazoweza kushuka daraja kutoka kwenye La Liga.

Kikosi hicho cha kocha Javier Aguirre kinahitaji ushindi kwenye mechi hiyo ili kuiweka mbali Cadiz isiifikie kwenye msimamo baada ya kuwashuhudia wapinzani wao hao wakipoteza mechi saba za mwisho na hivyo kuwapa matumaino wao ya kuponyeka na kubaki kwenye ligi.

Real Madrid ambayo imeshabeba ubingwa, haina presha yoyote hivyo kocha Carlo Ancelotti lazima atapumzisha wachezaji wake baada ya kazi ngumu waliyofanyika usiku wa Jumatano iliyopita kwenye mechi ya marudiano ya hatua ya nusu fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich.

Mechi ya wikiendi hii si muhimu sana kwa Real Madrid, lakini itakuwa na kitu kwa wapinzani wao, Granada. Matokeo yoyote zaidi ya ushindi kwa Granada yatawathibitisha wababe hao kushuka daraja, huku hatima ya Granada inaweza kufahamika mapema kabla ya mechi yao kuanza kama tu, Mallorca itaichapa Las Palmas. Mechi ya mwisho ya Jumamosi, itaishuhudia Athletic Bilbao ikikipiga na Osasuna.

Kesho, Jumapili kitapigwa kipute cha Cadiz na Getafe. Katika mchezo huo, Cadiz italazimika kukwepa kichapo kama inataka kuepuka kushuka daraja.

Atletico Madrid mchezo wao wa nyumbani dhidi ya Celta Vigo ni wa vita ya nafasi kwenye Top Four kwa vijana hao wa Diego Simeone. Lakini, Celta Vigo wao watahitaji pointi tatu ili kujihakikishia usalama baada ya msimu mgumu kwao.

Rayo Vallecano itasafiri kwenda Valencia katika mechi nyingine pia yenye mtazamo wa kusaka usalama kwenye hatari ya kushuka daraja. Mechi hiyo ni ya ushindi lazima kwa Valencia baada ya wikiendi iliyopita kukubali kipigo kutoka kwa Alaves, ambao iliwafanya wawe nyuma kwa pointi tano dhidi ya Betis, ambao kwa sasa wapo kwenye nafasi ya mwisho ya wenye uhakika wa kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao.

Betis inapaswa kuzoa pointi tatu kutoka kwenye mechi dhidi ya Almeria, ambao tayari imeshashusha daraja. Almeria ilishinda wikiendi iliyopita dhidi ya Rayo, hilo likithibitisha sawa wanashuka daraja, lakini bado wanapambana hadi mwisho.

FC Barcelona itasubiri hadi Jumatatu itakapojimwaga uwanjani Nou Camp kukipiga na Real Sociedad.

Kikosi cha Xavi kitahitaji kushinda mchezo huo ili kufufua matumaini yao ya kurudi kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa ligi na hilo linawezakana kwa kuzingatia matokeo ya Girona usiku wa jana, wakati Real Sociedad itaanza kwenye mechi hiyo ikiwa nafasi ya saba, nje ya michuano ya Europa League msimu ujao, endapo kama Betis itakuwa imechapa Almeria kesho, Jumapili.

Chanzo: Mwanaspoti