Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesho tutaweka historia mpya hapa Tabora - Kocha Goran

Goran Kopunovic 09 14.jpeg Kocha Mkuu wa Tabora United, Goran Kopunovic.

Fri, 15 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Tabora United, Goran Kopunovic leo Ijumaa asubuhi, Septemba 15, 2023 amezungumza na waadishi wa habari kuelekea mechi yao ya Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prison.

"Tunatambua utakua mchezo mgumu sana kesho dhidi ya Tanzania Prison lakini tumejiandaa vizuri. Huu ni mchezo wetu wa kwanza kucheza nyumbani katika msimuu huu na mchezo wa kwanza baada ya miaka tisa kupita timu ya Tabora kucheza katika uwanja huu.

"Tunahitaji kuweka historia nzuri baada ya mda mrefu kupita kwahiyo tunahitaji kupata ushindi. Mashabiki waje kwa wingi kutupa sapoti tuandike historia hii nzuri kwa pamoja," amesema Kocha Goran Kopunovic.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: