Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KenGold yatinga Ligi Kuu ya NBC

Kengold017 KenGold yatinga Ligi Kuu ya NBC

Sun, 21 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya KenGold kutoka mkoani Mbeya imepanda daraja kucheza Ligi Kuu ya NBC msimu ujao baada ya kufikisha alama 67 kileleni mwa msimamo wa Ligi NBC Championship, ambayo imebakiza raundi moja pekee kuhitimisha msimu.

KenGold imefikisha alama hizo baada ya leo kuifunga FGA Talents magoli 2-0, huku washindani wake, Pamba Jiji wakiwachapa TMA mabao 2-1 ugenini na Biashara United wakipokea kichapo cha 2-1 ugenini kutoka kwa Pan African.

Matokeo haya ya mechi za leo kwa washindani wa KenGold yanaifanya Pamba Jiji ambayo imefikisha alama 64 kwenye nafasi ya pili kuwa ndiyo timu pekee yenye uwezo wa kuifikia Kengold.

Kwa mujibu wa kanuni; Timu mbili za juu kwenye msimamo wa Ligi ya NBC Championship zitapanda daraja kucheza Ligi Kuu ya NBC, na timu mbili zinazofuata zitapitia mechi za mtoano, hivyo tayari Kengold ametangulia.

Wanaoweza kumfuata KenGold Ligi Kuu ya NBC ni ama Pamba Jiji au Mbeya Kwanza inayoshika nafasi ya tatu ikiwa na alama 62.

TIMU TANO ZA JUU 1. KenGod FC- 67 2. Pamba Jiji FC-64 3. Mbeya kwanza FC- 62 4. Biashara United- 59 5. TMA -54.

Kila timu imebakiza mechi moja kukamilisha msimu, Je, nani atamfuata KenGold Ligi Kuu ya NBC?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live