Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ken Gold warejea kileleni Championship

Ken Gold Kileleni Ken Gold warejea kileleni Championship

Sun, 29 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Ken Gold ya Mbeya jana imefanikiwa kupanda kileleni mwa Ligi ya NBC Championship baada ya ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Biashara United Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.

Mechi nyingine za Ligi ya NBC Championship, wenyeji Pan Africans waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fountain Gate Talents Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, wakati Cocpo ya Mwanza iliwalaza wenyeji, Ruvu Shooting 1-0 Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Ushindi wa jana unafanya Ken Gold ifikishe pointi 19 na kupanda kileleni mwa Ligi ya NBC Championship, ikiwazidi pointi mbili ndugu zao, Mbeya Kwanza baada ya wote kucheza mechi nane.

Copco imesogea nafasi ya saba baada ya kufikisha pointi 11, Pan Africans imesogea ya 13 baada ya kufikisha pointi saba, wakati Biashara United sasa ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi tisa, Ruvu Shooting yenye pointi moja inashika mkia na Fountan Gate Talents inashukia nafasi ya 12 kwa pointi zake nane baada ya wote kucheza mechi nane.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live