Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kelvin Yondani; Ng'ombe asiyezeeka maini

Kevin Yondani Cotton Juice Kelvin Yondani

Wed, 24 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nilimuona Kelvin Yondani akiwa na kitambaa cha unahodha wa timu yake Geita Gold. Ilikuwa siku chache zilizopita. Nikakimbilia katika mtandao wa Wikipedia kutazama umri wake.

Msela Kevin yupo uwanjani mpaka leo. Nadhani hata msimu ujao atakuwepo uwanjani. Jina? Kelvin Yondani. Tarehe ya kuzaliwa? Oktoba 9, 1984. Umri? Miaka 39. Bado Kelvin anadunda katika nafasi ngumu ya ulinzi wa kati. Akiwa katika umri huu amekumbana na kina Fiston Mayele, Prince Dube, Jean Baleke na wengineo.

Kwa mujibu wa mtandao huo huo wa Wikipedia inaonyesha kwamba John Bocco ambaye jina lake lipo katika usajili wa Simba msimu huu ana umri wa miaka 34.

Amepitwa miaka mitano na Yondani. Kwanini Bocco hayupo uwanjani? Kwa sasa nasikia anasomea ukocha huku akifundisha timu ya Simba chini ya umri wa miaka 17. Ni baada ya kumfukuza na kumwambia amezeeka katika soka letu.

Ni kitu ambacho tumekuwa tukifanya mara nyingi baada ya kumchoka mchezaji. Mchezaji mwenye roho ndogo huwa anakimbia akiambiwa hivi. Sana sana kama anacheza Simba au Yanga.

Huwa anaukubali uzee, anavunjika moyo, kisaikolojia anajiona mzee kweli. Inatokea sana kwa wachezaji wazawa. Wachache ndio wanaweza kuwa wabishi. Ni kama inavyotokea kwa Yondani.

Mpaka leo nina uhakika kwamba Bocco angeweza kwenda katika timu nyingine ya kawaida isiyo na presha. Angeweza kufunga walau mabao saba kwa msimu yangeitosha timu hiyo. Iwe Coastal Union au Namungo ama Tanzania Prisons.

Angeweza kufanya hivyo. Bocco angesimama mbele katika timu ambayo inamtegemea ambayo inaamini katika ustaa wake. Ambayo ina mashabiki wachache wanaomtegemea angeweza kurefusha urefu wa maisha yake ya soka mpaka kufikia miaka 40 kuliko kujidanganya kuwa kocha.

Edo Kumwembe, Mchambuzi wa Wasafi Media

Chanzo: www.tanzaniaweb.live