Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kelvin Mandla: Simba SC ni kubwa Afrika

Kelvin Mandla: Simba SC Ni Kubwa Afrika Kelvin Mandla: Simba SC ni kubwa Afrika

Fri, 18 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mpya wa Viungo Simba SC Kelvin Mandla amefunguka kwa mara ya Kwanza baada ya kutambulishwa rasmi na Uongozi wa Klabu hiyo jana Alhamis (Novemba 17).

Mandla ametambulishwa Klabuni hapo akichukua nafasi ya Kocha Sbai Karim aliyeoondoka na Kocha Mkuu Mserbia Ziran Maki mapema mwezi Septemba mwaka huu.

Kocha Mandla amesema amefurahi kujiunga na Klabu ya Simba SC ambayo imekua na muendelezo mzuri katika Michuano ya Afrika, huku akiahidi kujitoa kwa moyo wake wote ili kuiwezesha kupata mafanikio msimu huu 2022/23.

“Simba ni timu kubwa, ni timu ambayo sio tu inashiriki bali kushindana kwenye michuano ya CAF. Nitazamia kuungana nao katika jambo hilo na kusaidia timu kwenda mbele zaidi ya ambapo imewahi kufika,” amesema Mandla alipohojiwa kupitia Simba TV.

Kabla ya kutambulishwa kwa Kocha Mandla, Simba SC ilimtambulisha Kocha wa Makipa Chlouha Zakaria mwanoni mwa juma hili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live