Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kelvin John "Mbappe" ajiunga na Timu ya Daraja la Kwanza Denmark

Kelvin John Mbappe Denmark Kelvin John

Sat, 1 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania mwenye umri wa miaka 20, aliyekuwa akikipiga kwenye klabu ya KRC Genk, Kelvin John amejiunga na klabu ya AaB Fodbold inayoshiriki ligi daraja la kwanza maarufu kama NordicBet Liga ya huko nchini Denmark.

Mkurugenzi wa michezo wa AaB, Ole Jan Kappmeier amesema kuwa Kelvin John ni mchezaji wa mafanikio ambaye anaamini anaweza kujiendeleza zaidi akiwa klabuni hapo.

Aidha Mchezaji Kelvin John kupitia mazungumzo yake na AaB alisema;- “Mara ya kwanza kabisa AaB ilipoonyesha nia, nilidhamiria kuja hapa, na kupitia mazungumzo yangu na klabu nilipata taswira nzuri juu ya klabu hii na inanifaa kabisa”

“Natumai kwamba kwa kasi yangu, bidii yangu naweza kusaidia timu wiki baada ya wiki na wakati huo huo.

Kelvin amesaini mkataba wa miaka minne kuitumikia AaB hadi mwaka 2028 na atavaa jezi nambari 27 kuanzia msimu ujao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live