Shabiki maarufu wa Klabu ya Simba, Mjata Mjata amedai kuwa kuna wakati kelele za mashabiki na wachambuzi zinazisaidia klabu za Tanzania kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.
Mjata Mjata amesema hayo wakati akifanya mahijiano kwenye kipindi cha Kipyenge Extra cha EA Radio huku akiiytolea mfano Yanga kwa Club Africain msimu uliopita kwenye michuano ya Kombe la SHirikisho Afrika ambapo Yanga ilitoa sare nyumbani ikaenda kushinda ugenini na kusonga mbele mpaka fainali.
"Wakati mwingine tunatakiwa tuelezane tu ukweli, hizi hamasa tunazozizungumza na hizi kelele mashabiki sisi tunazozipiga kuna wakati mwingine zina faida.
"Mfano halisi, Yanga ilishawahi kucheza mechi moja na Club Africain hapa uwanja wa Taifa ikatoka sare, baada ya kutoka sare ikawa mtaani huku mashabiki wanavyoongea wakawa wanaongea kwa presha kubwa sana.
"Ikafika kipindi vile wanavyoongea mashabiki mtaani vikawafikia wachezaji na benchi la ufundi, mechi iliyofuata ambayo Yanga alienda kucheza Tunisia walishinda 1-0 akifunga Aziz Ki.
"Baada ya mechi kuisha Mayele alisema kwamba tulivyocheza mechi ya nyumbani baada ya kutoka sare tulipata malalamiko mengi sana kutoka kwa mashabiki, kwahiyo tulichukulia yale malalamiko kama deni na ndio maana leo tumeamua kulilipa," amesema Mjata Mjata.