Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kazi ipo! Mastaa hawa kustaafia wapi?

Kustaafu Pic Kazi ipo! Mastaa hawa kustaafia wapi?

Tue, 12 Apr 2022 Chanzo: Mwanaspoti

UTUMISHI wao katika timu mbalimbali walizotumika ikiwemo Stars, umewajengea heshima na walipata umarufu mkubwa ndani na nje, huku kazi zao zikibakia kumbukumbu kwa wanasoka chipukizi.

Hapa kinazungumziwa kizazi kilichoibuka miaka ya 2000, kilichofanya kazi iliyowatambulisha katika jamii na bado kimeendelea kukomaa kwenye gemu.

Swali ni je? mastaa hao watastaafu wakiwa na timu gani, kulingana na huduma zao kutumika timu mbalimbali za ndani na nje kama ilivyokuwa kwa Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga), Mussa Hassan Mgosi (Simba) hao ni baadhi ya walioagwa kwa heshima.

Mwanaspoti linakuchambuliwa mastaa ambao walivuma sana na bado wameendelea kukomaa kwenye gemu, huku kitendawili kikubwa ni wapi wataagwa kati ya timu walizozitumikia.

MBWANA SAMATTA-ANTWERP

Hajatumika na timu nyingi za Ligi Kuu Bara nje na African Lyon (2008/2010) na Simba(2010/11), hadi sasa ana miaka 11 akicheza nje, TP Mazembe ambapo alichukua tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa soka la ndani.

Hadi sasa nje amecheza timu tano ambazo ni TP Mazembe (2011-2016), Genk (6016–2020), Aston Villa (2020/2021), Fenerbahçe (2020/21) na sasa yupo kwa mkopo Royal Antwerp (2021/22), licha ya hilo swali ni je Samatta atastaafia wapi?

ERASTO NYONI-SIMBA

Kutokana na Nyoni kucheza nafasi tofauti ( namba 2,3, 4,5,6) na kudumu kwenye gemu akilinda kiwango chake, amekuwa funzo mbele ya chipukizi kuzingatia nidhamu ya soka.

Kapitia timu nyingi, baadhi ni Vital’O (2009), Azam FC (2010-2017) na aliiwezesha kunyakua taji la ubingwa wa ligi kuu 2014, Simba (2017-2022) ameiwezesha kutwaa ubingwa wa ligi mara nne, pamoja na wa ASFC na Kombe la Mapinduzi, pia amehudumu Stars kwa muda mrefu. Kwa sasa mkataba wake Msimbazi unamalizika.

JOHN BOCCO-SIMBA

Japokuwa hajacheza timu nyingi, utumishi wake ndani ya miaka tisa akiwa Azam FC (2008-2017), alichukua ubingwa wa ligi kuu 2014, ubingwa wa Kagame, Mapinduzi, wakati Simba ameongoza kutwaa mataji manne ya ligi kuu na ASFC tangu ajiunge nao (2017-2022), pia alikuwa bandika bandua Stars. Naye mkataba wake Msimbazi upo ukingoni.

KELVIN YONDANI-GEITA GOLD

Beki Kelvin Yondani amekuwa aikoni kwa chipukizi kupenda aina ya uchezaji wake, baadhi wakikiri wanatamani kufikia mafanikio yake, pamoja na heshima aliyoijenga akistafu soka atakuwa timu gani.

Aliitumikia Simba (2006-2012) na aliiwezesha kuchukua ubingwa wa ligi ndogo 2007 na 2010, 2012 wa ligi kuu, Yanga (2012-2020) aliisaidia kunyakua ubingwa wa ligi kuu 2013, 2015, 2016 na 2017, kisha akajiunga na Polisi Tanzania (2020/21), sasa yupo Geita Gold (2022).

HARUNA MOSHI ‘BOBAN’-KENGOLD

Kati ya vipaji vinavyotajwa kuwahi kutokea nchini, Haruna Moshi Boban ni mmoja wapo, baadhi ya wachezaji waliowahi kukiri hilo ni Shiza Kichuya, Atupele Green, Shaaban Kisiga waliostafu soka ni Amri Kiemba na Frank Kasanga ‘Bwalya’

Boban alizitumikia timu mbalimbali kama Moro United (2003/2004), Simba (2004-2009), aliisaidia kuchukua ubingwa 2009/2010, Gefle IF (2010/11), Simba (2011-2013), Coastal Union (2013-2015), Mbeya City (2015-2017), Friends Rangers (2017/18), Yanga (2017/18) na sasa yupo Kengold, licha ya utumishi wake je atatundika daruga akiwa na timu gani.

DANNY MRWANDA-KENGOLD

Ni kati ya mastaa waliyozitumikia timu nyingi na bado amekomaa kwenye gemu, akiwa na Kengold inayoshiriki ligi ya Championship.

Timu alizozichezea ni Arusha (2003-2005), Simba (2006–2008) aliisaidia kuchukua ubingwa 2007 wa ligi ndogo, Al Tadamon (2008/2009), Simba (2009/2010) aliiwezesha kuchukua ubingwa 2010.

Đong Tam Long An (2010-2012), Simba (2012/2013) alivaa medali ya ubingwa 2012, Da Nang (2013), Yanga (2014), Polisi Morogoro (2014/2015), Lipuli (2015/2016), Kagera Sugar (2016/2017), Majimaji (2017/2018), Njombe Mji (2018/2019), Mbeya Kwanza (2019) na sasa yupo Kengold (2022).

MRISHO NGASSA-KENGOLD

Ni winga mwenye rekodi ya mabao 25 Stars, akifuatia na Samatta (22), ameipa Yanga mataji ya ligi kuu 2008, 2009. Aliichezea Kagera Sugar (2005/06), Yanga (2007–2010), Azam FC (2010–2013), Simba kwa mkopo (2012/2013), Yanga (2013–2015), Free State Stars

(2015/2016), Fanja (2016/2017), Mbeya City (2017/2018), Ndanda FC (2018), Yanga (2018) baadae akajiunga na Gwambina na sasa yupo Kengold.

JUMA KASEJA-KMC

Ni kati ya makipa wenye heshima kubwa nchini, kabla ya Aishi Manula hajawa Tanzania One, alikuwa Juma Kaseja, ameipa Simba ubingwa 2003, 2004,2007 ligi ndogo, 2010, 2012 na Yanga aliiwezesha kutwaa ubingwa 2015.

Kaseja amecheza Moro United (2000-2003), Simba (2003–2014), Yanga (2014/2015), Mbeya City (2015–2017), Kagera Sugar (2017/2018) na sasa yupo KMC (2018-2022). Kaseja tayari ana taaluma ya ukocha, licha ya kuendelea kucheza.

WENGINE

Mbali na wakali hao orodha inayo pia kina Himid Mao, Azam FC, Petrojet, ENPPI na Ghazl Mahalla, Juma Nyoso kacheza Simba, Kagera Sugar, Friends Rangers, Ruvu na sasa yupo Geita Gold na Elias Maguli kapita Simba, Stand United, Dhofar ya Oman, KMC, Nakambala Leopards ya Zambia, FC Platinum ya Zimbabwe na sasa yupo Ruvu Shooting. Mchango wa mastaa hao kwenye soka la Tanzania, umemuibua mchezaji wa zamani wa Azam FC, Philippo Alando, kujiuliza mastaa hao ambao wana heshima yao kizazi cha sasa watastafia wapi. “Kuna wachezaji wamecheza Simba, Yanga na Azam FC kwa kiwango cha juu, mfano Bocco na Nyoni najiuliza na ulijendi wao watastafia wapi,” anasema Alando.

Chanzo: Mwanaspoti