Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaze awachimba mkwara Polisi

Kaze Pic CCCC Kocha Kaze

Fri, 16 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amemtaka kocha wa Polisi Tanzania Mwinyi Zahera kujiandaa na kichapo wakati timu hizo zitakapokutana kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara Desemba 17.

Akizungumza, kocha huyo amesema wachezaji wote wapo tayari kuikabili Polisi Tanzania isipokuwa Aboutwalib Mshery atakayekosekana.

“Tuna mheshimu Zahera alikuwa mwenzetu na ni kocha mwenye mbinu nyingi lakini Jumamosi atatusamehe sababu tunazitaka hizo pointi tatu ili kutimiza malengo yetu,” amesema Kaze.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliofanyika Agosti 16 uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha Yanga ilishinda mabao 2-1.

Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 38 baada ya michezo 15 wakati Polisi Tanzania ipo mwisho wa msimamo nafasi ya 16 ikiwa na pointi 9 baada ya michezo 15.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live