Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaze akafanye kazi Kagera

Cedrick Kazeeee Kocha Kaze

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea mchezo wa kesho Jumatano (Oktoba 04) wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar, Kocha Mkuu wa Klabu ya Namungo FC, Cedric Kaze, amesema ameimarisha safu yake ya ushambuliaji kuhakikisha hawapotezi mchezo huo.

Akizungumza baada ya kuwasili mjini Bukoba, Kocha huyo kutoka nchini Burundi amesema hana wasiwasi kwani makosa aliyoyaona kwenye mchezo uliopita ameyafanyia kazi.

“Kwa sasa timu yangu ipo vizuri nimefanya maandalizi ya kutosha ili tuweze kupata matokeo katika mchezo huo,” amesema Kaze.

Amesema wachezaji wote wanaendelea vema kiafya isipokuwa Paterne Counou ambao atakosekana kutokana na kuwa majeruhi.

Ameongeza kuwa anaiheshimu timu ya Kagera Sugar kwani ina wachezaji wenye Uzoefu, hivyo wanapaswa kuingia kwa tahadhari kubwa ili kupata matokeo mazuri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: