Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaze ahisi hujuma Yanga

Pic Kaze Data Kaze ahisi hujuma Yanga

Tue, 16 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

Mbeya. Kocha wa timu ya Yanga, Cedric Kaze amesema anajua wapo watu ambao wanataka timu hiyo isichukue ubingwa msimu huu, lakini hawawezi kuwa toa katika lengo lao la msingi.

Baada ya mchezo wao na Mbeya City kumalizika kwa sare ya bao 1-1, Kaze alisema kuna watu ambao wanataka kuwakatisha tamaa, lakini wao wanaendelea kupambana kwa ajili ya kutimiza kile ambacho wanakiamini kwa msimu huu na lengo kuu kwao.

“Kuna watu inaonekana kama wanataka kutukatisha tamaa, lakini sisi malengo yetu hayawezi kubadilika, zaidi tunaenda kujipanga na mechi zetu zijazo,” alisema kocha huyo raia wa Burundi.

Akizungumzia mchezo huo kiujumla, Kaze alisema katika kipindi cha kwanza walitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini hawakufanya hivyo, jambo ambalo pia lilichangia kuutia ugumu mchezo huo.

“Tulitengeneza nafasi nyingi sana katika kipindi cha kwanza lakini hatukutumia vizuri, hilo nadhani linatakiwa kufanyiwa kazi kwa ajili ya kuonyesha utofauti katika mchezo unaofuata,” aliongeza kocha huyo wa zamani wa vijana wa Barcelona.

Kwa upande wa kocha wa Mbeya City, Mathias Lule alisema kupata pointi moja kutoka kwa Yanga ni muhimu kulingana na timu waliyocheza nayo.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz