Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaze afunguka siri ya mafanikio ya Yanga

Fdgj Yanga Kaze Kaze afunguka siri ya mafanikio ya Yanga

Sat, 20 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze, amesema mafanikio makubwa ambayo timu hiyo imeyapata msimu huu yametokana na kuwa na idadi kubwa ya wachezaji wenye viwango vikubwa na vinavyofanana.

Akizungumza mara baada ya kuwasili Dar es Salaam jana wakitokea Afrika Kusini katika mechi ya marudiano ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Marumo Gallants ambapo walipata ushindi wa jumla wa mabao 4-1, Kaze, alisema msimu huu wamepata mafanikio kutokana na wachezaji wote kujituma kila walipopata nafasi.

Kaze alisema wachezaji wamepambana katika kila mechi na walikuwa wakionyesha ushirikiano ndani na nje ya uwanja.

"Yanga msimu huu tunajivunia kuwa na kikosi cha wachezaji wenye viwango vikubwa na vinavyofanana, akikosa huyu atacheza huyu, ukiwapumzisha hawa watacheza wengine na wanaoingia viwango vya havipishani na waliopumzika. Ndiyo maana utaona tunacheza vizuri kila mechi. Wachezaji wote waliosajiliwa wamechangia kwa asilimia kubwa na si kikundi tu fulani cha wachezaji na wengine wamekaa tu," alisema Kaze.

Kocha huyo raia wa Burundi alisema kama wangekuwa na sehemu tu ya wachezaji ambao ndiyo wana viwango vikubwa kuliko wengine, wasingefanya vyema katika mashindano ya kimataifa na kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

"Tumechukua ubingwa wa Tanzania Bara, tuko nusu fainali ya Kombe la FA na fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, hii inaonyesha tuna wachezaji bora na wanaofanana na kukaribiana sana viwango, vinginevyo hali isingekuwa hivi. Angalia mfano tumecheza Jumatano iliyopita Afrika Kusini, tumesafiri, tumefika Dar, tutapanda ndege kwenda Dodoma, halafu tutasafiri tena kwa basi kwenda Singida ili tucheze nusu fainali.

Siku ya Jumapili tuna mechi ya fainali dhidi ya USM Alger, nakwambia kama una wachezaji hao hao unakwama, lakini kama kawaida sisi tutatumzisha baadhi ya wachezaji, tutachezesha wengine ambao uwezo wao ni sawa tu na waliopumzika," alisema Kaze.

Yanga inatarajia kujiandaa kuwakaribisha USM Alger kutoka Algeria katika mechi ya kwanza ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika itakayochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Waalgeria hao wamesonga mbele katika michuano hiyo baada ya kuwaondoa ASEC Mimosas kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: