Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema wanaruhusu vijana walioko timu za vijana wakosee ili waweze kuwakosoa na kuwasashihisha kutokana na makosa yao. Amesema hayo wakati wa mahojiano na waandishi wa Habari mara baada ya mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya KMKM uliochezwa Uwanja wa Amaan Zanzibar ambapo waliamua kuwapa nafasi vijana waonyeshe vipaji vyao. “Tumeamua kuwapa nafasi vijana ili waonyeshe vipaji vyao na tuwaruhusu wakosee ndio tuwakosoe na kuwafundisha kwani watajifunza kutokana na makosa yao na kufanya vizuri naamini wamefanya kile kilicho katika uwezo wao kwa kufanya kile walichotakiwa kufanya .anasema Kaze na kuongeza; “Mchezo wetu unaofuata ni dhidi ya Singida na tunawafahamu vizuri wachezaji tulionao ni hao hao tunaamini tuna njia nzuri ya kufanya vizuri dhidi yao na kusonga hatua inayofuata ya nusu fainali ya michuano hii. Yanga wanatarajia kesho kushuka dimbani kuwavaa Singida Big Stars wenye pointi 3 sawa na Yanga katika mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi ambapo mmoja atasonga mbele katika hatua ya nusufainali.