Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaze: Yanga waliiga Prisons

C76ec0ebc71174e81273abfc72f9c631 Kaze: Yanga waliiga Prisons

Fri, 8 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KOCHA wa Yanga Cedric Kaze alisema kuiga mbinu za wapinzani wao ni sababu iliyowafanya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Tanzania Bara, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga, Rukwa.

Alisema kwenye mchezo huo wapinzani wao walikuwa wanatumia mbinu ya kupiga mipira mirefu mbele, wachezaji wake waliiga mfumo huo ambao uliwatibulia mipango ya kupata ushindi.

Akitoa tathimini mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Kaze alisema malengo yao yalikuwa kwenda kushambulia kupitia pembeni, lakini wachezaji wake walipoteza muelekeo baada ya mbinu yao kushindikana.

“Kipindi cha kwanza tulifuata mchezo wao, malengo yetu yalikuwa ni kushambulia kupitia pembeni ili kupata nafasi ya kwenda kufunga, lakini kitendo cha kuwaacha kutangulia kutufunga walituharibia mbinu, kwani ilitakiwa kupambana kutafuta bao la kusawazisha,”alisema Kaze.

Alisema pamoja na matokeo hayo ya mechi ya ugenini, bado kikosi chake kipo kwenye muelekeo mzuri, kikubwa ni kupigania ubingwa, hivyo wanaenda kujipanga kwa mchezo unaokuja kuhakikisha wanarejesha makali yao.

“Mashabiki wawe na subira kwani wanajua timu inakotoka tunaenda kujipanga kwa mchezo unaokuja kuhakikisha tunafanya vyema,”alisema

Naye kocha wa Tanzania Prisons, Salum Mayanga amewapongeza wachezaji wake kwa kupambana na kufanikiwa kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Yanga.

Alisema Yanga ni timu nzuri yenye rekodi nzuri tangu walipoanza ligi, licha ya kwamba wachezaji wake walifanya makosa mengi, lakini walicheza na kutoa upinzani aliotarajia kuuona kwenye mechi hiyo.

Yanga mchezo unaokuja wanatarajia kucheza dhidi ya Mbeya City wakati Tanzania Prisons watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya KMC.

Chanzo: habarileo.co.tz