Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaze: Tunakuja kivingine

Kaze Pic Data Kaze: Tunakuja kivingine

Mon, 1 Mar 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Oliver AlbertMore by this Author MASHABIKI wa Yanga licha ya kuchekelea timu yao ikitinga 16 Bora baada ya jana kuifunga Ken Gold ya Daraja la Kwanza kwa bao 1-0 katika mechi ya Kombe la Shirikisho (ASFC), ila bado wanaonekana kutoridhishwa na kiwango cha baadhi ya nyota wao, lakini kocha wao, Cedric Kaze amewatuliza akiwaambia wasihofu kwani, mambo matamu yanakuja.

Yanga ilipata ushindi huo kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam kwa bao la mkwaju wa penalti kupitia mshambuliaji wao mpya, Fiston Abdulrazack, lililokuwa la kwanza kwake katika mechi za mashindano tangu asajiliwa mapema mwezi uliopita.

Penalti hiyo ilipatikana dakika ya 42 baada ya Boniface Mwanjonde kuunawa mpira katika harakati za kuokoa na mwamuzi Ahmed Ajariga kutoka Manyara kutoa adhabu hiyo na Fiston kupiga kiufundi kuiandika Yanga bao pekee kwenye mchezo huo uliokuwa mkali.

Ushindi huo umeifanya Yanga kuungana na watani wao, Simba kutinga hatua ya 16 Bora, lakini baadhi ya mashabiki waliohudhuria mchezo huo wamesikika wakilalamikia umakini mdogo wa nyota wa kikosi chao kilichowafanya washindwe kutokana na kapu la mabao mbele ya Ken Gold.

Hata Kocha Kaze naye aliliona jambo hilo na kukiri anajipanga na kubadilisha mbinu zake ili mambo yawe matamu zaidi Jangwani katika mechi zao zijazo ikiwamo ile ya Alhamisi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz