Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaze: Tuko tayari kuwavaa Coastal Union

Kaze Pic CCCC Kaze: Tuko tayari kuwavaa Coastal Union

Mon, 19 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Msaidizi wa Klabu ya Young Africans, Cedric Kaze amesema kuwa kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union ambao unatatajiwa kupigwa kesho Jumanne ya December 20, 2022, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo huo, Kaze amesema mara nyingi Coastal Union ni timu inayowapa changamoto kila wanapokutana nayo.

Lakini anaamini Yanga iko kwenye wakati mzuri zaidi kuwakabili wagosi hao wa kaya wenye makazi yao Jijini Tanga.

“Tuna deni na mashabiki wetu kwenye mbio za ubingwa, naamini tuko vizuri kuwakabili Coastal Union, timu ambayo inatupa ushindani mkubwa kila tunapokutana,” alisema Kaze

Kaze ameongeza kuwa pamoja na Coastal Union kutokuwa na matokeo mazuri katika msimu huu, timu hiyo ina wachezaji wengi wenye vipaji, hawapaswi kuwadharau

Akizungumzia utayari wa kikosi chake, Kaze amesema kuwa ukimuondoa mlinda lango wao nambari mbili Aboutwalib Mshery ambaye ni majeruhi, mwingine ni winga Tuisila Kisinda aliyepata changamoto katika mchezo dhidi ya Polisi Tanzania na baada ya mazoezi ya mwisho leo, watafanya tathmini kuona kama ataweza kutumika hapo kesho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live