Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaze: Simba wepesi tu, tatizo Chama, Luis

Kaze 2 Pic 1 Data Kaze: Simba wepesi tu, tatizo Chama, Luis

Mon, 15 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

By Mwandishi WetuMore by this Author KATIKA toleo la jana katika mahojiano maalumu na Cedric Kaze, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga aliyefurushwa wiki iliyopita, tuliona akianika kirusi kinachoitafuna timu hiyo ya Jangwani.

Alifafanua, pia juu ya ukweli wa kukwamishwa mambo mengi aliyokuwa akiyatengeneza na wachezaji wake kwa ajili ya kuifanya Yanga iwe moto na kueleza ni kazi kubwa hata kwa kocha ajaye kama ‘kirusi’ kilichopo klabuni hapo akitadhibitiwa ili mambo yaende sawa.

Katika kuhitimisha makala iliyotokana na mahojiano hayo maalumu, Kaze ameichambua Simba na kudai mechi baina yao kwake ilikuwa ndio mechi nyepesi sana, lakini kinachoiangusha Yanga ni kule kukosekana kwa watu wenyewe uwezo mkubwa kama kina Clatous Chama na Luis Miquissone. Kivipi? Endelea naye...!

UBORA WA SIMBA

“Unajua watu wanashindwa kuelewa, Yanga haiwezi kuwa bora kwa siku moja. Hivi unakumbuka Simba ilikotoka unakumbuka kina Laudit Mavugo, Emmanuel Okwi, Charles Ilanfya, Haruna Niyonzima, Joseph Owino wale Wabrazili, Waghana na wengine ambao nimewasahau hao wote walicheza Simba kwa vipindi tofauti, wakati huo ilikuwa inajaribu. Haikuwa inajua itafikia hapa ilipo sasa,” anasema na kuongeza;

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz