Kocha msaidizi wa Kikosi cha Yanga, Cedrick Kaze amesema kuwa mechezo wa leo dhidi ya Marumo Gallants ni wa kujitoa mhanga.
Kaze amesema hayo akihojiwa na vyombo vya habari Afrika Kusini kuelekea mchezo huo wa Nusu Fainli ya Kombe la Shirikisho Afrika.
"Tumemaliza mazoezi lakini pia tumejiandaa kwa kila kitu ambacho kinaweza kutokea uwanjani, tunaamini ni dakika 90' za mchezo mgumu.
"Marumo wanapenda kucheza pasi fupi fupi, skills na spidi hivyo vyote tumeviona kwenye mechi ya kwanza lakini kesho mi mchezo wa kujitoa muhanga.
"Kesho ni dakika 90' za kuweka historia kwahiyo kila mtu anatakiwa kujitoa kuanzia dakika ya kwanza," amesema Kaze.