Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaze: Malalamiko yanavunja moyo wachezaji

Kaze Yanga Cedrick Kaze

Tue, 10 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Msaidizi wa Yanga Sc, Cedrick Kaze raia wa Burundi amesema malalamiko amesema malalamiko ya baadhi ya mashabiki yanavunja moyo wachezaji wa timu hiyo.

Kaze amesema hayo jana Jumatatu, Mei 9, 2022 baada ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons ambao ulipigwa katika Dimba la Mkapa na kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Hii ni mechi ya tatu mfurulizo sasa kwa Yanga katika Ligi hiyo wakicheza bila kuibuka na ushindi ambapo hali hivyo imeanza kuibua mijadala kuwa huenda ndoto za ubingwa zikaanza kufifia kutokana na kupunguza kasi huku Ligi ikielekea mwishoni.

“Matokeo mabaya ni kweli yanaumiza hata sisi makocha hakuna anayefurahia kuona timu yake haipati matokeo mazuri, tunaumia sana lakini hatuna jinsi, cha msingi tunaangalia mechi zijazo tufanye vizuri.

“Najua wanaumia sana kuona timu haifanyi vizuri lakini wajue Mungu huenda kuna kitu kikubwa ametuandalia huko mbele, habari za kulalamika hadi kupitiliza sio vizuri zinatuvunja moyo wachezaji,” amesema Cedrick Kaze.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live