Mshambuliaji wa Singida Fountain Gate, Francy Kazadi amezungumza kuhusu ukame wa mabao alionao tangu alipojiunga na timu hiyo Januari mwaka huu katika dirisha dogo la usajili baada ya kutamba katika Kombe la Mapinduzi 2023 alipoibuka mfungaji bora akifunga mabao sita.
Katika kipindi cha miezi minane ambayo Kazadi ameitumikia Singida, timu hiyo imecheza mechi 15 msimu uliopita na mechi mbili za Ligi Kuu msimu huu na mbili za hatua ya awali Kombe la Shirikisho Afrika.
“Mungu akitenda miujiza naweza kumaliza na mabao 20 msimu huu," amesema nyota huyo wa zamani wa AS Vita kuzifumania nyavu akitaka kuvunja rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa Somba, Meddie Kagere aliyefunga mabao 22 msimu wa 2019/20.