Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kay Mziwanda awapopoa vigogo Simba anguko la Simba

Kay Mziwanda Na Ahmed Ally Kay Mziwanda awapopoa vigogo Simba anguko la Simba

Wed, 29 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki maarufu wa Simba SC, Kay Mziwanda amewachana viongozi wa Simba SC kuwa ndio sababu kubwa ya anguko la Simba msimu huu.

Kay ametoa kauli hiyo mara baada ya Simba kucheza mechi ya mwisho ya msimu kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar dhidi ya JKT Tanzania na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa 2-0..

"Hili anguko la Simba hata tusitafute mchawi, Meze wetu Mangungu hata hahusiki, ni viongozi ambao ndio wanahusika na usajili, wametuletea wachezaji ambao hawana uwezo wa kupambana kama vile Jobe, yule ni mchezaji wa mpira au mwanariadha?," alihoji Kay.

Kay alimaliza kwa kuwataka viongozi kujitathimini kwani kwa misimu mitatu sasa wamekuwa wakifanya makosa yaleyale hivyo wanapaswa kuiachia timu kabla mashabiki hawajachukua hatua abaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live