Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kauli zamponza mtangazaji Olimpiki

Medaliiiiiiiiiiiiiiiiii Kauli zamponza mtangazaji Olimpiki

Tue, 30 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mtangazaji mkongwe wa michezo ameondolewa katika kazi yake kwenye Olimpiki ya Paris baada ya kutoa maoni ya ubaguzi wa jinsi kuhusu waogeleaji wa kike wa Australia walioshinda medali ya dhahabu.

Wakati vimwana wa timu ya mashindano ya 4x100m freestyle wakitoka kwenye bwawa la mashindano mjini Paris, Bob Ballard alisema “unajua, wanawake wapo kwa ajili ya kukaa tu, kujipamba kwa vipodozi“.

Video hiyo haraka ikazagaa na warushaji wa matangazo Eurosport baadaye wakasema mtangazaji huyo ameondolewa.

Ballard bado hajazungumzia kauli yake iliyomponza.

Waogeleaji wa kike, Mollie O’Callaghan, Emma McKeon, Meg Harris na Shayna Jack walikuwa wametoka kuwashinda washiriki wa timu ya Marekani na China, na kuiwezesha Australia kushinda medali ya dhahabu ya shindano hilo kwa msimu wa nne mfululizo.

Walikuwa wakipungia mikono mashabiki na kusherehekea mafanikio yao wakati Ballard alipotoa kauli hiyo.

Mtangazaji mwenzake, mwogelea bingwa wa Uingereza, Lizzie Simmonds haraka aliponda kauli ya Ballard.

Jumapili, Eurosport ilisema Ballard – mwandishi na mtangazaji wa siku nyingi wa BBC – atarejea kazini.

“Wakati wa matangazo ya Eurosport wa jana, mchambuzi Bob Ballard alitoa maoni ambayo hayako sahihi,” kampuni hiyo ya kurusha matangazo ilisema katika taarifa yake.

“Kutokana na hilo, ameondolewa miongoni mwa timu ya wachambuzi mara moja.”

Ballard amekuwa mtangazaji mkubwa wa michezo hiyo ya kimataifa tangu miaka 1980, akiripoti Michezo ya Olimpiki mingi na Mashindano ya Dunia mara nyingi.

Chanzo: Mwanaspoti