Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kauli ya Zoran baada ya kusepa Simba

Zoran Maki 1 1140x640 1 Zoran Maki

Wed, 7 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba, Zoran Maki ameibuka na kuishukuru klabu hiyo kwa imani kubwa iliyompa ikiwa ni muda mchache tangu kuachana nayo.

Taarifa iliyotolewa na Klabu hiyo kupitia kwa Ofisa Mtendaji wake Mkuu, Barbara Gonzalez ilieleza kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba na Zoran ikiwa ni miezi miwili tu tangu alipochukua mikoba ya Mhispania, Pablo Franco aliyeondoka Mei 31, mwaka huu.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Zoran aliandika; "Napenda kuishuruku klabu hii kwa kunipa nafasi ya kipekee, asante kwa wote walioniamini na ninashukuru kwa kila kitu,"

Msimu huu pekee kwenye michezo ya Ligi Kuu Bara aliyokiongoza kikosi hicho, Zoran ameshinda yote akianza na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold Agosti 17 kisha ushindi wa 2-0 kutoka kwa Kagera Sugar Agosti 20 yote ikichezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live