Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kauli ya Yanga baada ya kipigo cha Ihefu

IHEFU VS YANGA LEO.jpeg Kauli ya Yanga baada ya kipigo cha Ihefu

Wed, 30 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kupoteza mchezo wa jana wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu FC kikosi cha Yanga kimewasili salama Dar.

Novemba 29/2022 itakuwa kwenye rekodi ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi kuonja joto ya kupoteza mechi ya ligi kwa mara ya kwanza tangu itunguliwe Aprili 25,2021.

Timu ya mwisho kuifunga Yanga ilikuwa ni Azam FC kwenye mchezo wa ligi uliokamilika kwa ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Yanga 0-1 Azam FC kwa bao la Prince Dube.

Novemba 29,2022 ubao wa Uwanja wa Highland Estate, Mbeya ulisoma Ihefu 2-1 Yanga na kuwafanya wadondosje pointi tatu mazima.

Ni mabao ya Nivere Tigere na Lenny Kissu yaliwatuliza Wananchi huku bao la Yanga likifungwa na kitasa Yannick Bangala.

Miongoni mwa wachezaji walioanza kikosi cha kwanza cha Yanga ni pamoja na mtupiaji wao namba moja Fiston Mayele mwenye mabao 10, Dickson Job na Kibwana Shomari kwa upande wa mabeki.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa wanajivunia rekodi ambayo wameweka ni jambo la kuwapongeza wachezaji na benchi la ufundi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live