Saa chache baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Try Again kujiuzulu, Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu naye ameibuka na kutoa kauli yake.
Alipotangaza kujiuzulu Try Again hapo jana Juni 11, 2024 alisema anampendekeza rais wa heshima na Mwekezaji Mohamed Dewji awe Mwenayekiti wa Bodi wakati yeye anapoachia nafasi hiyo lakini hata hivyo, Mangungu amekwenda tofauti katika hilo.
“Hakuna wasiwasi wowote wa Wajumbe ambao wameamua kujiuzulu kwasababu wamejipima na wameona wanahitaji changamoto mpya, hivyo Wajumbe wengine watateuliwa upande wa Mwekezaji, waje tuchague Mwenyekiti mpya wa Bodi na tufanye kazi”
“Suala la Try Again kujiuzulu na kumpendekeza MO kuwa Mwenyekiti wa Bodi ni maoni yake binafsi nje na utaratibu wa Kikatiba, Mwenyekiti wa Bodi anachaguliwa na Wajumbe wa bodi kwa kupigiwa kura hivyo tutamchagua Mwenyekiti wa Bodi kwa mujibu wa Katiba," alisema Mangungu.