Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kauli ya Kocha Nabi kwa KMC

Nabi 3 1320x943 Kocha Nabi akizungumza

Wed, 26 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea mchezo wa leoi dhidi ha KMC FC, Kocha Mkuu wa Yanga SC, Nasredinbe Nabi amesema kwa sasa klabu inakumbwa na ratiba ngumu kutokana na michezo mingi kufuatana ndani ya kipindi kifupi.

“Tunafahamu kuwa ratiba yetu ni ngumu, tunafanya kila jitihada kwendana na uhalisia unaotukabili kwa sasa. Tuna mechi ngumu mbele yetu na huo ndio ukweli ambao tunapaswa kupambana nao. Sio suala la nani atacheza ni suala la alama tatu.”

Kocha amesema anawaheshimu KMC FC kutokana na matokeo yao ya hivi karibuni ikizingatiwa walitoa sare na Simba Sc na kuifunga Azam Fc kwa bao 2-1.

“KMC FC ni timu nzuri tunapaswa kuwaheshimu. Wameonesha upinzani mzuri kwenye mechi zilizopita bila shaka ufanisi wao ni mzuri. Tuna muda mchache wa kujiandaa lakini alama tatu kwetu ni muhimu,” alisema Nabi.

Hata hivyo nyota wetu Chrispin Ngushi amerejea rasmi kikosini baada ya kukaa nje kwa muda mrefu. Vile vile Ngushi amegusia kuhusiana na mchezo ujao dhidi ya KMC FC.

“Timu imejiandaa vizuri licha ya kuwa tumetoka kwenye mchezo mgumu. Tuna muda mchache sana kujiandaa kwa ajili ya mchezo ujao lakini tumejiandaa vyema, kuwakabili wapinzani wetu. Tunawaheshimu KMC FC kwa sababu ina wachezaji wazuri lakini tuna imani tutashinda” alisema Ngushi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live